Wanafunzi wa Tanzania wanaosomea Jiangxi, wameshiriki Maonesho ya Kitamaduni ya Kimataifa International Cultural Festival (ICF) yaliyofanyika tarehe tarehe 14 Novemba, 2020 nchini China.
Maonesho hayo ambayo hufanyika
mara moja kwa mwaka yalifadhiliwa na Chuo Kikuu cha Jiangxi cha masuala ya
Fedha na Uchumi (JUFE) ambapo yaliwakutanisha wanafunzi wanaoziwakilisha nchi
zao, wafanyabiashara na raia mbalimbali wa nchini China.
Katika maonesho hayo wanafunzi
wa Tanzania waliweza kuonesha fursa za uwekezaji na biashara katika bidhaa za
Korosho, Utalii, mapishi ya chakula cha asili cha Tanzania na madini ya
Tanzanite ambapo banda la Tanzania lilikuwa ni miongoni mwa vivutio kutokana na
maandalizi yake ambapo lilihusisha utalii wa Tanzania kwa kuonesha picha za
video na vipeperushi vilivyotolewa na ubalozi wa Tanzania nchini China.
Katika maonesho hayo kundi
la wanafunzi wanaosomea Uzamili kutoka Tanzania ambao pia ni watumishi wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na afisa biashara
kutoka wizara ya Viwanda na Biashara ndugu, David Geofrey walishiriki kuandaa
banda la Tanzania.
Wanafunzi wa kitanzania wanasoma nchini China katika picha ya pamoja waliposhiriki maonesho ya Kitamaduni ya Kimataifa International Cultural Festival (ICF).
![]() |
| Bango likionesha vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini Tanzania. |
Raia wa China wakiwa katika banda la Tanzania kuona vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini Tanzania katika maonesho ya Kitamaduni ya Kimataifa International Cultural Festival (ICF).


