Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amefanya kikao na wamiliki na wasimamizi wa
Viwanda vinavyotengeneza malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono ( Hand Sanitizer).
Lengo la kikao hicho
ilikuwa ni kujadiliana na wenye viwanda, wazalishaji pamoja na wadau wengine
watakavyoweza kuongeza uzalishaji ili kufanikisha upatikanaji wa vifaa kwa
ajiri ya kujikinga na usambaaji wa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona
(COVID19).
Katika kikao hicho Kampuni
la Kilombero Sugar imetoa lita 30,000 za alcohol bure kwa serikali zitaakazosaidia
kutengeneza vitakasa mikono (Hand sanitizer) ili kusaidia juhudi za serikali za
kupambana na virusi vinavyosababisha ugojwa wa Corona. Pia kampuni ya Consumer
Choice Ltd imetoa kwa serikali kiasi cha lita 10,000 za ethanol na pia imeamua
kubadili matumizi ya Ethanol ambayo yalipaswa kutengeneza vilevi ambapo
asilimia 75% za Ethanol zitatengeneza vitakasa mikono (hand sanitizer) na 25% ya
Ethanol itakayobaki itatumika kutengeneza vilevi. Kampuni ya Mount Meru
Millers imetoa lita 10,000 ya Vitakasa mikono (Hand sanitizer) itakayosambazwa
kwa vituo vya afya na taasisi nchini.
Waziri wa Viwanda na
Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) amewataka wenye viwanda kuongeza
uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vitakasa mikono pia amewaelekeza TBS na
FCC kuendelea kukagua wafanyabiashara wa vitakasa mikono ambao wanauza bidhaa
feki na hafifu pia kwa wote wanaopandisha bei kwa lengo la kujinufaisha
kuwachukulia hatua kali za kisheria kwani wanahatarisha maisha ya watanzania.