Search This Blog

Wednesday, February 5, 2020

Mapokezi ya Katibu Mkuu, Prof. Riziki Shemdoe



MAPOKEZI YA KATIBU MKUU MTEULE PROF. RIZIKI SHEMDOE

Dodoma. Katibu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amewataka wafanyakazi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii, weledi na uadilifu ili kuyafikia matarajio ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati unaotegemea Viwanda ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza na watumishi hao kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu Prof. Shemdoe alimshukuru Mhe Rais kwa kumuamini na kumteua na kumuona anafaa kuongoza Wizara hiyo,

Prof. Shemdoe aliwataka watumishi kumpa ushirikiano wa kutosha katika utendaji wa kazi kama walivyoonesha ushirikiano kwa Katibu Mkuu mstaafu. “Hii ni wizara iliyobeba ajenda ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya nchi yetu kuwa ya viwanda ili kukuza uchumi na kuchochea maendeleo ya watu hivyo tujue sisi tumepewa jukumu kubwa ambalo tunapaswa kufanya ili wizara hii itoe matokeo yanayotarajiwa na Mhe. Rais Magufuli.  “Nawahakikishia kuwapa ushirikiano na wakati wote ofisi yangu itakuwa wazi bila kikwazo chochote muda wote nitapatikana nitakapohitajika.

Akielezea matarajio yake kwa watumishi hao Prof. Shemdoe aliwataka kusimamia ajenda ya Tanzania ya Viwanda na pia anatarajia kuwa watafanya kazi kwa uharaka na ufanisi.

Naye Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake Prof. Joseph Buchweishaija alimpongeza Prof. Shemdoe kwa kuteuliwa kuongoza Wizara hiyo.
“Nampongeza Prof. Shemdoe kwa kuteuliwa kuongoza Wizara hii, hii ni wizara yenye watu wanaojituma na kufanya kazi kuanzia uongozi wa juu hadi wafanyakazi wa chini”.
Akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Bw. Ludovick Nduhiye alieleza kuwa lengo la kikao hicho ni kufahamiana na kutambuana na alihaidi kufanyika kwa kikao kingine cha kujadili mambo mbalimbali ya kiutendaji na changamoto za watumishi.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi (TUGHE) Wizara ya Viwanda alielezea kuhusu umuhimu wa baraza la wafanyakazi katika kupitisha bajeti ya Wizara.
“Ulidokeza kuhusiana na maandalizi ya bajeti  ya Wizara, Tunatakiwa kupata wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, tunarajia mwezi huu wa pili kamishina wa kazi atakuja kwa ajili ya kufanya uchaguzi ili baade baraza hilo liweze kupitisha bajeti ya Wizara kama ilivyo utaratibu”.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe akisalimiana na kaimu mkurugenzi idara ya maendeleo ya Viwanda ndugu Leo Lyayuka mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara Mtumba jijini Dodoma.


Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe na watumishi katika ofisi za wizara Mtumba, jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe akisaini kitabu katika ofisi yake Mtumba, jijini Dodoma.


Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Joseph Buchweishaija akikabidhi ofisi kwa Katibu mkuu mteule Prof. Riziki Shemdoe katika ofisi za wizara Mtumba, jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na wafanyakazi katika ukumbi wa chuo kikuu cha Dodoma.



 Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wizara ya viwanda na biashara akiongoza mkutano kati ya Katibu mkuu wa wizara ya viwanda na watumishi wa wizara kilifanya katika ukumbi wa chuo cha UDOM.



Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Joseph Buchweishaija akizungumza wakati wa kuwaaga watumishi wa wizara ya viwanda na biashara.



Picha ya pamoja ya Katibu mkuu wizara ya viwanda na watumishi wa wizara hiyo.



Baadhi ya watumishi wa wizara wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu Prof. Shemdoe.



Prof. Kitila Mkumbo aanza kazi muda mchache mara baada ya kuapiswa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Profesa Kitila Alexander Mkumbo kuwa Waziri wa Viwanda n...