Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki S. Shemdoe Leo tarehe 3 Septemba, 2020 ameongoza kikao cha Kamati ya Uongozi (Steering Committee) ya Uwezeshaji Biashara katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jijini Dodoma.
Lengo la kikao hiki
lilikuwa ni kujadili utekelezaji wa maelekezo ya mkutano wa kwanza wa kamati
hiyo uliofanyika tarehe 13 Februari 2020.
Masuala yaliyojadiliwa na
kuidhinishwa ni pamoja na hadidu za rejea (ToR) za kamati ya kitaifa ya uwezeshaji
biashara, Maeneo ya kundi A, B na C ya mkataba wa uwezeshaji biashara wa
Shirika la Biashara la Dunia (WTO TFA) ambayo yatawasilishwa sekretarieti ya
WTO kabla ya tarehe 22 Septemba, 2020.
Utekelezaji wa masuala
mengine ya biashara nje ya mkataba wa uwezeshaji biashara, utekelezaji wa mpango mwelekeo (Roadmap) wa miaka mitano
(2020/21 - 2024/2025) na mpango kazi (Action Plan) ya mwaka 2020/2021. Aidha,
Kamati imetoa maelekezo ya maboresho ya Mfumo wa taarifa za ufanyaji biashara
(National Trade Information Module) kabla ya kufanyiwa uzinduzi rasmi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Mwinyi Talib Haji akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jijini Dodoma.
