Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Geofrey Idelphonce Mwambe (Mb) na Naibu Waziri wa Wizara ya
Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe (Mb) leo tarehe 10 Desemba,
2020 wameripoti katika ofisi za wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma na
kupokekewa na Menejimenti ya Wizara hiyo ikingozwa na Katibu Mkuu Prof Riziki
Shemdoe na Naibu Katibu Mkuu ndugu Ludovick Nduhiye.
Wakizungumza na Menejimenti
hiyo baada ya kufika ofisini hapo wote kwa pamoja wameomba ushirikiano mkubwa kutoka
kwa Watumishi wote wa wizara huku wakisisitiza weledi na kujituma kwenye kazi
kwa kila mmoja ndio siri ya mafanikio.
Akizungumza katika kikao
kifupi na watendaji hao, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Mwambe amewataka
watumishi wote wa Wizara ya Viwanda kuumpa ushirikiano na kufanya kazi kwa
kutumia taaluma zao na kuhaidi kufanya kikao kingine na wafanyakazi wote ili
kujua changamoto mbali mbali zinazowakabili
watumishi na kuzifanyia kazi.
"Tunashukuru kwa
mapokezi yenu yaliyojaa upendo, tunawaahidi ushirikiano, tutafanya vikao na
taasisi zetu zote 15 zilizo chini ya wizara na kuzungumza na Wakurugenzi wakuu
wa taasisi na pia wakuu wa Idara na vitengo" Alisema Mhe. Mwambe.
Aidha Mhe. Mwambe aliwataka
wakuu wote wa Idara zinazosimamia taasisi hizo kuhakikisha zinaleta tija kwa
Taifa letu na watanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Naibu
Waziri, Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe (Mb) amewaomba watumishi wote wa wizara
hiyo kumpa ushirikiano kwa kuwa yeye ni mwenyeji
katika Wizara hiyo na kuwataka watumishi
wawe tayari kuendana na mabadiriko yalitokea na kuahidi kuwa atafanya
kazi kwa weredi bila kumuonea mtu wala kuumpendelea mtu.
"Niwaombe tushirikiane
kama Timu ili tuweze kufika tunapopataka, kwenye sekta zetu hizi yapo mambo
ambayo yaliahidiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa
kuomba kura kwa wananchi na yapo kwenye Ilani ya CCM, ni kazi yetu kwenda
kuyasimamia na kuyatekeleza kama yalivyoelekezwa" Alisema Mhe. Kigahe.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara
ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amewapongeza Mawaziri kwa kuteuliwa
kwao na kuwakaribisha huku akihaidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa viongozi hao
katika kuijenga Tanzania ya Viwanda.
![]() |
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geofrey Idelphonce Mwambe (Mb) pamoja na Naibu waziri Mhe. Exaud Kigahe (Mb) baada ya kupokelewa na Katibu wa wizara Prof. Riziki Shemdoe pamoja na Naibu Katibu Ludovick Nduhiye na watumishi wa wizara.
![]() |
| Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geofrey Idelphonce Mwambe (Mb) akisalimiana na wafanyakazi wa wizara mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara zilizoko Mtumba jijini Dodoma. |
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geofrey Idelphonce Mwambe (Mb) akisaini katika ofisi za wizara Mtumba na kufanya majadiliano na Naibu waziri pamoja na Katibu Mkuu pamoja na Naibu Katibu Mkuu.



