MHE. INNOCENT BASHUNGWA AONGOZA MAMIA
YA WATANZANIA KATIKA MKESHA WA KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA KATIKA KUUKARIBISHA
MWAKA MPYA 2020.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameongoza mamia ya watanzania
katika mkesha wa kuliombea Taifa la Tanzania uliofanyika usiku wa Jumanne tarehe
31 Desemba, 2019 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Katika
mkesha huo wa kuukaribisha mwaka mpya 2020 uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali
wa serikali na wa dini ambapo waliongoza kwa dua na maombi kuliombea taifa
letu, hasa viongozi waliobeba dhamana ya kuwatumikia watanzania ili waweze
kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Akihutubia
umati huo, Mhe. Bashungwa ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, alisema kwamba lengo la Serikali ya
awamu ya tano ni kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinatumika kunufaisha Watanzania.
Katika kufanikisha hilo, Serikali inaendelea kujenga miundombinu wezeshi
ikiwemo barabara, maji, umeme, huduma za afya, elimu n.k
Aidha
Mhe. Bashungwa alisema kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha rasilimali za
kilimo na utalii zinanufaisha wananchi walio wengi na sio wachache. Akitolea
mfano kwenye sekta ya viwanda na biashara, maboresho yamefanyika BRELA, TBS na
EPZA na kubainisha kuwa tayari fidia imekwishalipwa kwa ajili ya kujenga eneo
maalumu la uchumi Kurasini litakalotumika kuchakata mazao ya kilimo na
kutengeza ajira kwa kina mama na vijana ili kukuza uchumi wa nchi.
Katika
mkesha huo Askofu Mkuu wa Tanzania Fellowship of Church (TFC) ndugu Godfrey
Malasi alisema kuwa viongozi walioteuliwa na Mhe. Rais Magufuli, wana jukumu la
kumsaidia huku wakiendana na kasi ya awamu ya tano na sio kumbebesha mzigo kwa
kutotimiza wajibu wao kiutendaji.
Malasi alisema kuwa uelewa
mdogo wa wananchi katika kusaidia kusukuma kasi ya uchumi wa viwanda imekuwa ni
changamoto katika kuongeza kasi ya maendeleo kwani wamegeuka kuwa wachuuzi
badala ya wazalishaji wa bidhaa hizo.
Alisema kuwa
kauli
mbiu ya Tanzania ya viwanda inamtaka kila mmoja kushiriki kikamilifu na siyo
kuzurura mtaani ukiuza vifaa vya urembo badala ya kwenda kulima na kuzalisha
mazao.
“Neno la Mungu linasema
asiyefanya kazi na asile, ukimuona mtu ananing’iniza ushaga mwambie aende
vijiji akalime tupate mazao sababu mambo ya kuning’iniza shanga haliwezi kuleta
mabadiliko yoyote kwenye Tanzania ya viwanda,” alisema
Mkesha huo wa Kitaifa
uliandaliwa na kuratibiwa na mashirika ya dini (Tanzania Fellowship of Churches)
kwa Kushirikiana na Makanisa na huduma mbalimbali.
MWISHO
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Habari na Mawasiliano,
Wizara
ya Viwanda na Biashara,
31
Desemba, 2019
