Naibu Katibu Katibu Mkuu, Lodovick Nduhiye, tarehe 8 Oktoba, 2020 Ameshiriki uzinduzi wa Kiwanda cha kuchakata pamba cha chama kikuu cha Ushirika (KACU LTD) Kilichopo wilaya ya Kahama.
Katika ufunguzi huo Naibu Katibu Mkuu alipata fursa ya kutoa saamu za wizara kwa kupongeza chama cha ushirika kwa hatua hiyo waliyofikia ya kuwa na Vinu vya kuchambulia pamba (ginnery) ambavyo vitasaidia katika kazi kuchambua pamba na kuongeza uzalishaji.
Aidha ameupongeza uongozi wa Kiwanda kwa juhudi kubwa wanazofanya kwani kwa hatua hiyo waliyofikia watasaidia ajira kwa watanzania wenzetu wa Kahama na mikoa ya jirani.
![]() |
| Naibu Katibu Mkuu Ludovick Nduhiye akitoa salamu za Wizara katika hafla ya ufunguzi wa kiwanda cha kuchakata pamba cha Chama Kikuu cha Ushirika (KACU LTD) kilichopo Wilaya ya Kahama. |
