![]() |
| Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara akiongoza majadiliano kwenye kikao chake na Wamiliki na Wasimamizi wa Viwanda vya Samaki Jijini Mwanza |
MKUTANO WA WAMILIKI NA WASIMAMIZI WA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA
ZIWA
Mhe. Innocent
Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara leo Desemba 8, amekutana na kufanya kikao
na wamiliki na wasimamizi wa viwanda vya samaki vilivyopo Kanda ya Ziwa Jijini
Mwanza.
Kikao hicho
ambacho pamoja na mambo mengine, kililenga kwenye kubaini changamoto mbalimbali
zinazowakabili wenye viwanda na hatimaye kutafuta ufumbuzi wa pamoja na
Serikali kiliandaliwa chini ya mwamvuli wa Chama cha Wasindikaji Samaki na
Kampuni za Uvuvi za Viwandani yaani kwa Kiingereza, Tanzania Industrial Fishing
and Processors Association (TIFPA).
Baadhi ya changamoto
na kero ambazo wadau hao walizibaini kuzuia maendeleo ya viwanda vya samaki nchini
ni pamoja na usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi na nyaraka za kuuza nje, marejesho
ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) pamoja na ushuru mkubwa.
Mhe. Bashungwa yuko
Jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajia kutembelea viwanda
vilivyopo Jijini humo, na kuzungumza na wafanyakazi ili kubaini changamoto
zinazokabili viwanda vya ukanda wa Ziwa Victoria, vilivyopo Jijini humo.
MWISHO
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Viwanda na Biashara,
08 Desemba, 2019
![]() |
| Mhe. Bashungwa akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau wa Viwanda vya Samaki Jijini Mwanza. |





