![]() |
| Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara akisalimiana na Mhe.Pham Minh, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam leo tarehe 10.12.2019 |
Mhe. Innocent Bashungwa
Waziri wa Viwanda na Biashara leo tarehe 10 Desemba 2019, amekutana na kufanya
mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti kutoka Vietnam Mhe.
Pham Minh na ujumbe wake kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini
Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao ambayo
yalijikita kwenye misingi na umuhimu wa ushirikiano wa kidugu baina ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na nchi ya Vietnam, Mhe. Bashungwa alitumia fursa hiyo
kumshukuru mgeni huyo na Serikali ya Vietnam kwa kununua Korosho ya msimu
2018/2019 zaidi ya asilimia 70 ya mzigo uliokuwepo.
Naye Mhe. Minh, kwa upande
wake aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha mahusiano mazuri
hususan kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho ndio kinachoongoza Serikali
nchini.
MWISHO
![]() |
| Viongozi wakiwa kwenye mazungumzo pamoja na wajumbe waliohudhuria wakifuatilia mazungumzo hayo. |




