MKUTANO WA WAMILIKI WA VIWANDA VYA NYAMA NA NGOZI
Wizara
ya Viwanda na Biashara inapenda kuwafahamisha wenye Viwanda vya Nyama, Ngozi
pamoja na wadau wote wa sekta hiyo kuwa Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa
Viwanda na Biashara anatarajia kukutana na wadau wa sekta hiyo Alhamis tarehe 05
Desemba, 2019, kuanzia saa 5.30 asubuhi katika ukumbi wa Mikutano uliopo ofisi
za Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
Madhumuni ya mkutano ni kujadili mikakati
mbalimbali ya Serikali inayowekwa kwa ajili ya maendeleo ya sekta hiyo na wadau
husika. Kwa maelezo zaidi wasiliana na
Wizara, Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
MWISHO
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Viwanda na Biashara,
03 Desemba, 2019