Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa alipata wasaa wa kutembea mitaani na kuingia mwaloni Mwanza kwa mguu kuangalia hali ya biashara hasa ya mnyororo wa thamani wa samaki aina ya sangara na kubadilishana mawazo na wafanyabiashara wadogo wa maeneo hayo na wavuvi.
"Nimejifunza kwamba hakuna kinachotupwa, hadi uti wa
mgongo wa samaki unatumiwa kusagwa na kuchanganywa na chakula cha kuku. Ni muhimu kuweka mwalo katika hali ya usafi na kusimamia mnyororo wa thamani wa sangara kuhakikisha tunapata maximum value ya kumnufaisha mvuvi, mfanyabiashara na mapato ya Serikali"
![]() |
| Mhe. Bashungwa akiwa kwenye picha na wafanyabiashara ya samaki alipotembea kwa miguu sokoni humo ili kujionea mnyororo wa biashara ya samaki na mapato yanayopatikana |



